Manifestation Through Walking (Kumanifest Jambo kwa Kutembea)

Rakims
0

Manifestation through walking ni njia rahisi ya kudhihirisha malengo yako kwa kuunganisha mwili, pumzi na nishati ya ardhi kupitia kutembea peku. Njia hii ya manifestation inakusaidia kuunganisha na Mother Nature na kuongeza nguvu ya kiroho.

Mwanafunzi na Mwalimu

Mwanafunzi:

Mwalimu ni Amali gani iliyo pure yenye faida zaidi ambayo naweza kufanya bila ingredients na kablasha zingine.

Mwalimu:

Manifestation.

Mwanafunzi:

Sasa hii mwalimu sindio zile zile utaanza kusema sema maneno?.

Mwalimu:

Umetaka simple na pure hivyo nielewe hapa.

Si kila manifestation ni lazima utegemee chanting kuna muda chanting (Nyiradi) inajitegemea pia na manifestation (Kudhihirisha) kunajitegemea pia.

Sasa kwa hapa fuata hatua hizi ambazo ni sehemu zako za maisha kila siku lakini unazienda kitofauti na mazoea yako ya kila siku.

HATUA ZA KUFUATA

  1. Nenda popote ambapo ni tulivu au sehemu watu wanatumia kufanya mazoezi hususani ya kutembea
  2. Hakikisha sehemu hiyo inakuruhusu kuwa peku mfano (Kando ya bahari)
  3. Tafuta nguo ambazo zitakufanya kuwa huru na zitakazo kuweka comfortable wakati unafanya zoezi lako.
  4. Anza kutembea hatua 20 kwenda na hatua 20 kurudi ulipotoka
  5. Hatua unazopiga ukipiga moja vuta pumzi ndani na ukipiga nyingine toa pumzi nje
  6. Endelea hivyo hadi utakaposkia miguu yako imeanza kuhisi uhai wa ardhi kuwa sasa unakanyaga kilicho hai chini kulingana na connection za pumzi zako kwenda chini.
  7. Jinsi Mguu wako utakavyokuwa unahisi mitetemo ya ardhi hapo hapo peleka command kwenye miguu yako ya nini hasa unataka. Utakikamilisha kwa muda usiotarajia

Note;

  • Zoezi hili si lazima kufanya kila siku
  • Zoezi hili si lazima kulifuatia sheria na taratibu
  • Zoezi hili ni kubwa sana

Wapo watu wanadanganya kuwa wanaenda Africa kutalii. Lakini wanakwenda Africa kwa ajili ya kuzungumza na Mother African Land (Mama wa Ardhi ya Afrika) ardhi pekee ambayo ni chanzo cha nishati za kiroho.

Hivyo usione wale wanaotembea tembea kando ya bahari peku wakiwa na Rangi nyeupe na mwendo wako ni kama kichaa kakosa mwenyewe ukahisi labda lile wanafanya ni Walking Exercise si kweli.

Anza na wewe kudanganya Rafiki zako kuwa unaishi kitourist wakati unaongea na mother nature. 🗺️


Manifestation through Walking

Ayah: 20 Surah Ankabut

Tembeeni katika Ardhi na Tazameni jinsi alivyo anzisha uumbaji.

Kisha Mwenyezi Mungu ndiye anaye umba umbo la baadaye.

Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza Juu ya Kila Kitu.

Quoted by;

Rakims Spiritual.


Rakims Spiritual.

manifestation through walking, spiritual manifestation, walking meditation, barefoot grounding, earth energy connection, law of attraction, africa spirituality, rakims spiritual

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !