Lucid Dreams na Faida Zake: Ndoto za Faida
Lucid Dreaming (Uelewa Ndotoni)
Lucid Dreams ni pale mtu anapoota na kujua kwamba anaota, yani yupo ndotoni. Na ndani ya ndoto ile akajielewa kuwa humu naota na kufahamu kwamba hapa nilipo nimelala na humu nilimo ni ndotoni, na kuanza ku-enjoy mazingira ya mule ndotoni na kufanya mengi atakayo.
Lakini pia kuna watu huota na kujijua kwamba wanaota bila mazoezi ya Lucid Dreams, lakini inakuwa sio kama Lucid Dream vile utakavyo vifanya. Hakuna tatizo lolote unaloweza kulipata ndotoni kwa maana ni ubongo wako ndio ufanyao kazi.
Soma pia: Manifestation Through Walking
JE NI FAIDA ZIPI ANAZOZIPATA LUCID DREAMER?
- Maajabu na miujiza kibao
- Kuzishinda ndoto za kutisha
- Ubunifu na kuondosha matatizo
- Kujiponya
- Mambo mengi yaliyopita
- Kupata muongozo what it was meant to be
- Kuliwazika na ndoto zake
- Kuongeza uelewa wa maisha yake ya kimapenzi
- Kupata uchangamfu siku nzima
- Kusaidia kuwasiliana na roho za waliotangulia mbele za Mungu
- Kwa wanaofanya meditation huwasaidia kuongeza awareness katika meditation
Zipo faida nyingi lakini hizo ni chache zibebazo topic......
Kwanini Nifanye Lucid Dreams?
Ni swali la wengi lakini chunguza faida zake zikikuvutia utafanya, lakini pia hukusaidia kufanya mengi ambayo unawish ungeweza kuyafanya katika ulimwengu wa kawaida kama vile:
- Kupaa
- Kupongezwa
- Kupata chochote kile unachohisi in real world hukipati
Wengi huingia kuuliza power zao wapi wataweza kuhunt money na starehe, lakini kuna mazuri zaidi ya hayo. Kwanza ukishajua hapa naota na nimo ndotoni utatamani uzunguke dunia nzima. But mengi huwa ni kweli kwa maana unakuwa in spirit form au thought, waweza kwenda popote, kula lolote na kufanya chochote. Kuna faida nyingi sana. Do it and you will feel it.
Soma pia: Njia Rahisi ya Kudhihirisha Bila Chanting
Vivutio vya Wengi in Lucid Dream World
1: Maajabu na Miujiza
Hii huwavutia wengi kuingia kudiliki kufanya mazoezi ya lucid na kufanya maajabu mengi ya ndotoni.
Wengi hudiliki kutoa hadithi walizotengeneza kwenye Lucid Dreams na kuziandika in real world kama:
1: The Wachowskis
Alieandika movie ya Matrix kama umewahi kuiona.
2: Lewis Carroll
Alieandika novel ya Alice in Wonderland.
Tafuta hizo movies na novels pia zitakupa idea kuhusu Lucid Dream.
2: Kuzishinda Ndoto za Kutisha na Kipumbaff
Hapa unakuta unaota unafukuzwa let say mfano unahisi kukimbizwa na watu na huu ni ugonjwa wa wengi let say umeweza kuingia Lucid Dream State.
Na ukajijua unaota. Wengi wakijua wanaota huanza kupigana na majinamizi au wachawi hao, ambayo pia inakuwa ni ujinga hali ume-realize unaota. Unasimama tu unaamrisha zina disappear na unaamuru nini cha kufanya au kujiamsha. Nice isn’t it?
3: Problem Solving
Wengi matatizo yakiwakaba hukimbilia kusubiri itakavyokuwa lakini ni udumazaji wa mawazo. Ukiingia Lucid na kuanza kujisolvia tatizo lako utapata muongozo. Mwisho wa siku unafanikiwa?
Je wajua niliwahi kujifunza kingereza cha kuunga unga kupitia Lucid Dreams???
4: Healing / Kujiponya
Let say umeumwa kichwa au mwili mzima. Kwa wanaofanya meditation, tuassume unaumwa malaria. Unaingia Lucid hukusaidia ku-open Third Eye na kufungua chakra zingine if only unameditate in dream na umelala unaota umelala chali. You will wake up healed or reduce pain maana tunaumia kutokana na ubongo kutambua tumeumia, na hatufanikiwi kutokana na ubongo umeamua hatufanikiwi kweli.
Ni maelezo marefu, mengine tutaendelea. Naangalia itapokelewa vipi hii mada hapa kwanza.
JINSI YA KUFANYA LUCID DREAM KWA BEGINNERS
Waweza kujiandalia mazingira yako ya kupata lucid dream na ikaleta effect upesi zaidi. Unachotakiwa kufanya ni kuandaa daftari lako la kufuatilia ndoto unazoota na mara kitu kikikutokea cha ghafla penda sana kujiuliza, “Hivi naota au?”
Penda sana pindi unapojiangalia kwenye kioo ukijiona jiulize pia, “Naota au?” Lakini ukiiona sura yako kwenye kioo means huoti na usipoiona jua upo ndotoni. Ni ngumu kidogo kujua kama unaota au laa lakini kwa mazoezi utajua tu.
Hatua za Kufuata
- Utatakiwa upate kitabu cha ndoto zako counter book dream journal
- Saa ya alarm
- Weka daftari yako pembeni ya ulalapo ili uweze kuandika kila kitu ambacho utaota usiku wote
- Angalia kitabu chako, kioo na saa yako mara kadhaa kwa siku
- Ukienda kulala jiambie: nikiota leo lazima nijue
- Tegesha alarm yako mapema zaidi ya kawaida, ikilia subiri dk kama sita halafu urudi tena kulala
- Ukihisi umeingia kwenye Lucid Dream jaribu kupaa juu juu ili kuthibitisha hili
Paa juu ya milima. Pia jaribu kupika hesabu ambazo huwa zinakushinda na maswali yakushindayo kujibu. Jaribu kufikiria ndugu yako gani umpendae ametangulia mbele ya haki na kuongea nae. Akirespond kile umemuuliza basi jua unaanza kuingia Lucid Dream World.
N.b
Jambo la kuzingatia hapo ni pale unapoenda kulala hakikisha hujikuni ovyo wala kujigusa gusa popote. Ukilala lala ubavu mmoja huo huo ili uweze kufanya mwili ujue umelala hali ya kuwa upo macho.
Soma pia: Kuunganisha na Nishati ya Ardhi
Rakims Spiritual.
