Kujua Jambo Kabla Halijatokea?
Yawezekana umewahi kusikia au kukutana na mtu anayesema aliwahi kuona jambo kabla halijatokea. Inaweza kuwa ni wewe mwenyewe au rafiki yako. Na ukichunguza, baada ya muda jambo hilo hutokea kweli.
Kujua hivyo ni moja kati ya nguvu za kiroho ambazo kila mtu anazo, lakini hutegemea na uwezo wake umeegemea upande gani.
Katika makala hii, tutachambua kwa undani aina mbalimbali za nguvu hizi na jinsi ya kujua ipi unayo.
Aina za Nguvu za Kujua Yajayo
- Prophecy (Unabii)
- Precognition (Kuona yajayo kupitia ndoto)
- Dejavu (Kuhisi tukio kabla halijatokea)
- Second Sight (Maono ya ghafla)
- Clair Audience (Kusikia sauti za yajayo)
1. Prophecy (Nguvu ya Kinabii)
Unabii ni nguvu ya kiroho inayohusishwa na Mitume. Mtu mwenye nguvu hii hupokea ujumbe mzito na wa uhakika kuhusu yajayo.
Kwa mujibu wa imani nyingi, mlango wa unabii ulifungwa baada ya Mitume wa mwisho. Hivyo, ni muhimu kutofautisha kati ya unabii halisi na madai ya uongo.
2. Precognition
Hii ni nguvu ya kuona mambo yajayo kupitia ndoto au hali ya nusu usingizi.
Watu wengi hupata ndoto ambazo baadaye hutokea katika uhalisia.
Dalili zake:
- Kuota jambo kisha linatokea kweli
- Kuota tukio lisilo na maana ya moja kwa moja lakini linajirudia
- Kuhisi tukio kabla halijatokea
Kwa mfano, unaweza kuota tukio la kawaida kabisa, na baadaye ukajikuta linaendelea kama ulivyoota.
Hii ni dalili ya precognition.
3. Dejavu
Dejavu ni hali ya kuhisi kwamba tukio linaendelea tayari uliwahi kuliona au kulipitia.
Hutokea ghafla wakati tukio linaendelea, na unaweza kuhisi kama unajua kitakachofuata.
Inashauriwa ukiipata hali hii, endelea na unachofanya bila kujaribu kuizuia.
4. Second Sight
Hii ni uwezo wa kuona tukio kabla halijatokea kupitia maono au hisia kali.
Watu wengine hupata hisia za ghafla kuhusu jambo linalokuja kutokea.
5. Clair Audience
Hii ni hali ya kusikia sauti zinazokuongoza kuhusu jambo linalokuja kutokea.
Inaweza kuwa kwa upole au kwa ukali, na mara nyingi hutokea katika hali ya utulivu.
Angalizo: Sauti hizi zinaweza pia kuwa za kupotosha, hivyo ni muhimu kuwa makini.
Wasiliana Nasi
Ikiwa unapendezwa na makala hizi, unaweza kuendelea kutufuatilia au kuwasiliana nasi kwa ushauri zaidi.
Email:
Rakimsspiritual@gmail.com
WhatsApp:
+255 788 485 293
Rakims Spiritual.
