MJUE KISISINA | MAALIM KISISINA | MCHAWI KISISINA

Rakims
1

KISISINA NI NANI?


Katika makala hii nitakuandikia au kukukumbusha kuhusu Kisisina yawezekana ikawa ni hadithi ya kusisimua kwako ambayo umewahi kuisoma au kusimuliwa yawezekana uliipenda au haukuipenda lakini katika makala hii kuna kitu utajifunza kuhusu KISISINA.


Je, Kisisina ni nani? 

Huyu alikua ni tabibu au mganga wa kienyeji katika karne zilizopita wengine hutoa hadithi yake kwa kusema Kisisina alikuwa ni jini lakini kwa makala nyingi zinamuandika kuwa alikuwa ni mwanadamu aliyepewa elimu ya Uganga na Uchawi ambapo alipewa uwezo huo na Mwenyezi Mungu (haijulikani aliokota au alifundishwa kupitia vitabu vya kale kabla yake).

 Alipewa uwezo wa kila jambo ambalo mwanadamu na majini walikua wanakwenda kwake ili kutatuliwa shida zao.
Kiukweli elimu yake hakuitumia vibaya kwa sababu ilikua imekamilika na ni elimu aliyopewa na Mwenyezi Mungu ili iwafae watu na majini.

kwa jinsi alivyopata elimu hiyo ilichukua muda kwa sababu jinsi alivyokua akipokea ndivyo alivyokuwa akiandika kwenye kitabu chake. Hadi pale alipoweza kufikia kuikamilisha kwa muda mrefu hivyo kutokana na kuwasaidia watu na uwezo wake kwenye fani hiyo kuzidi kuwa kubwa haitambuliki alikosea wapi! Lakini alielekea kufanya matendo yaliyokaribia kukufuru. 

Mwenyezi Mungu akajua umefika muda wa kuondosha elimu aliyokuwa kampa Maana kila kitu anawekea mwanzo na mwisho wake.

Na ilifikia sehemu watu wakaaanza na kumsahau Mungu wao na kuona mategemeo yao yote yapo kwa KISISINA hivyo watu wakaanza na kumsahau Mungu wao aliowaumba.

Hivyo basi ilipofika muda Mwenyezi Mungu akamtuma Malaika wake Jibril(Gabriel) A.S na kwenda kwa Maalim Kisisina kwa umbile la kibinaadamu akagonga hodi! na kukaribishwa na Maalim Kisisina.

Malaika wa Mungu Jibril A.S (Gabriel).

Akaulizwa:
 
''Ipi shida yako"? 

Akamwambia: 

"Mimi nimekuja kuangalia katika ramli yako uniambie huyu malaika (Gabriel) Jibril A.S yupo wapi?"

Kisisina akamwambia: 
"Ondoa shaka nitakutazamia" 

Lakini cha ajabu Kila Kisisina alipokuwa anaangalia kwenye kitabu chake akawa anamuona huyo mgeni wake ndio malaika mwenyewe Jibril (Gabriel).

Kila akirudia kupiga anakuta jibu linatoka ni huyo aliyopo mbele yake.

Kisisina akamwambia malaika wa mungu:

"nimeangalia mbingu zote, ardhi zote, Mashariki Magharibi, Kaskazini na Kusini simuoni Malaika Gabriel".

Akaendelea kusema;
"Sasa, kama Malaika Jibril sio mimi hapa basi ni wewe" 

Basi malaika Jibril A.S kufumba na kufumbua akampokonya kitabu kisisina na kupaa nacho mbinguni ila kwa uwezo na elimu aliyokuwa kapewa Kisisina ulivyokua mkubwa akipaa nae paka karibia mbingu ya saba malaika akamuomba Mwenyezi Mungu msaada afanye nini maana anaweza kuiingia mpaka mbingu ya saba.

Mwenyezi Mungu akamuamrisha malaika achane ukurasa mmoja kisha atupe  ndio malaika akafanya hivyo Mwenyezi Mungu alivyomuamrisha.

 alipotupa tu kile kipande yule Maalim Kisisina akashuka kukifata uku akijua ni kitabu kizima kumbe ni kurasa moja.

Malaika akaingia na Kitabu ndani ya mbingu ya Mwenyezi Mungu.

Kisisina baada ya kushuka paka chini kuangalia vizuri La hasha! kumbe ni karatasi moja alipo muangalia malaika kisha potelea mbinguni muda mrefu.
 
alikasirika sana na kuamua kutunga tena kitabu chake ambacho aliweka vitu vingine ambavyo vina uongo ndani yake na kuanza kuwafundisha watu pia.

JAMBO LA KUJIFUNZA KATIKA HADITHI YA KISISINA NI NINI?

Awali ya Yote tunatambua kuwa Uchawi na uganga upo na wapo walionao katika ukweli wake na wapo walionao katika uongo wake wapo walionao katika kusaidia na wapo walionao katika kuharibu
Upo mweupe (wa kutibu) na upo Mweusi (wa kudhuru).

FAIDA KATIKA HADITHI HII

  • Kuna ujumbe hapa kuhusu amali za kiroho
  • Kuna hekima inayotumika kabla ya kufanya maamuzi
  • Malaika ni wenye uwezo mkubwa lakini hawatendi ila kwa amri ya Mungu
  • Ukiwa na Elimu kubwa Jitahidi kuwa unawatenga watu kwa muda ili kurudi katika uhalisia
  • Hakuna kitu kitakaa milele.
  • Ukihisi unajua yote basi kuna wanaojua zaidi.
  • Dunia ina elimu nyingi sana ambazo hata kwa kuzijua majina yake hutomaliza
  • Hata uwe ni mtu wa aina gani Mungu akitaka kukupa anakupa tu.
  • Ukiwa na elimu na kitu unaweza kufanya chochote/lolote
MASWALI YA KUJIULIZA KUHUSU HADITHI HII

Je, ni kweli uchawi/nguvu ya aina hii ipo? 
Je, ikiwa mwanadamu kapewa elimu zaidi anaweza kuwazidi malaika?
Je, kwa nini watu hupinga elimu za kimajini na utabibu na hali ya kuwa zamani zilitumika katika manufaa?
Je, Mungu hakujua kama kisisina atatumia elimu vibaya?

Ikiwa mchawi anatuma nyoka kudhuru na nabii Mussa alipewa idhini ya kutupa fimbo yake iwe nyoka na kumeza nyoka wengine!
Wewe ukiwa na elimu ya Nyoka kukulindia shamba lako ni uchawi?
Hawakuwa mitume pekee waliopewa nguvu za miujiza kuna watu wapo walipewa na wengine tunao hadi leo, Je sio Baba zetu waliita manabii wachawi kwa kutuonyesha muujiza dhahiri?

Swali la mwisho la kujiuliza ni kuwa ikiwa Ramli ni haramu kwa nini basi malaika alikubali kupigiwa Ramli kwanza kabla ya kuchukua kitabu (Kulikuwa na hekima gani?)

Hekima ya Mwalimu Rakims Spiritual

Fahamu ya kuwa;
Mambo yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, Basi kama vile alivyokuwa akidanganywa mtoto kwa manufaa ya mzazi wake; 

Usitoke nje utaliwa na jitu, Nae ikachorwa hivyo hivyo kwenye DNA yake basi ni ukoo wake mzima atakao uzaa wataogopa kutoka nje usiku wataliwa na jitu.

Rakims Spiritual
Ni sehemu pekee utakapo kuwa unafunguka akili pole pole kuliko akili zako za degree na masters na mwisho wa siku hutavaa kanzu, suti au joho ili kuwa strong bali popote pale ulipo mradi unapumua utaendelea kupata nguvu ambayo baadae watu watakuuliza hii inatoka wapi.

Kwa haya na mengineyo jiunge na group yetu ya updates kupitia 👇👇👇

Rakims Spiritual Updates WhatsApp📱
Makundi

Chapisha Maoni

1Maoni

  1. Ukweli upo na kuna siku utadhihirika tu, mimi nimeanza kujifunza upya, mambo ya ushabiki nimeweka chini kwanza. Naam, hadithi za mtume ni haqqi lakini ni bora mtu akaangalie na mbadala wa mambo ya dini

    JibuFuta
Chapisha Maoni

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !