Muda Sahihi wa Kufanya Meditation kwa Matokeo Bora

Rakims
0

Muda Sahihi wa Kufanya Meditation

Jinsi muda unavyoathiri mafanikio ya meditation yako

Umuhimu wa Muda

Jambo la muhimu kabisa la kuzingatia unapoanza meditation ni muda.

Yeyote anayeanza meditation kwa mara ya kwanza anatakiwa kuwa na ratiba maalum ya muda wa kufanya meditation.

Meditation inayozingatia muda huwa na matokeo bora zaidi kuliko ile isiyozingatia muda.

Tazama mwongozo huu wa kina wa jinsi ya kufanya meditation hasa kama unahisi umekwama au unatafuta mwanga wa ndani.

Muda Unaopendekezwa

Unaweza kufanya meditation kwa muda usiopungua dakika 20 kila siku.

Kwa matokeo ya haraka zaidi, inashauriwa kufanya meditation mara mbili kwa siku:

  • Asubuhi
  • Usiku kabla ya kulala

Matumizi ya Alarm

Ni muhimu kuwa na saa maalum ya alarm kwa ajili ya meditation.

Epuka kutumia alarm ya simu, badala yake tafuta alarm maalum ambayo itatumika kwa meditation pekee.

Hii itasaidia akili yako kuzoea sauti hiyo na kuanza kuitambua kama ishara ya kuanza au kumaliza meditation.

Umuhimu wa Sauti ya Alarm

Hakikisha sauti ya alarm yako si ya kawaida au ile unayoisikia mara nyingi.

Kadri unavyoendelea kufanya meditation kila siku, akili yako itaanza kujitune na sauti hiyo na kuijua kama sehemu ya ratiba yako ya meditation.

Hitimisho

Kuzingatia muda ni moja ya siri kubwa za mafanikio katika meditation. Nidhamu ya muda itakuwezesha kupata matokeo bora na ya haraka zaidi.

Unahitaji ratiba kamili ya meditation?

Chat WhatsApp: +255 788 485 293

Shirikisha wengine 👇

Share WhatsApp

Rakims Spiritual

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !