Jinsi ya Kuanza Meditation ya Mwili (Mwongozo Kamili kwa Wanaoanza)

Rakims
0

Unataka kujua jinsi ya kuanza meditation ya mwili? Katika mwongozo huu kamili, utajifunza hatua kwa hatua namna ya kufanya meditation, faida zake, na jinsi ya kuunganisha mwili wako na akili kwa usahihi.

Tukianza na meditation

Mwongozo wa kuanza safari ya meditation kwa msingi sahihi

Utangulizi
Kabla ya kufanya meditation unatakiwa kuwa mwenye kujiandaa kwa vitu vitatu muhimu: kimwili, kiroho na kiakili.

Kwanza kabisa awali ya yote kabla ya kufanya meditation unatakiwa kuwa ni mwenye kujiandaa kwa vitu vitatu.

  1. Kimwili
  2. Kiroho
  3. Kiakili

Meditation Sahihi hufanywa kwa kufuata mpangilio wa muhusika katika sehemu hizo 3 hivyo ikiwa unataka kuanza safari ya meditation basi moja kwa moja tutaanza safari ya kimwili:

Meditation ni Elimu ambayo inataka msomaji kusoma hali ya kuwa anafanya vile vile. Ili uweze kuwa Master wa meditation.

Fahamu ya kuwa meditation inataka daily practices na sio kwa siku baadhi au kwa muda baadhi ambao umefanya eti tu kwa kuwa umepata muda wa kufanya.

Hili somo litakushinda mapema sana.

Meditation humtaka mwenye kujifunza kuwa ni mwenye kuiexperience pia ili kwenda nayo sawa. Ikiwa unasoma meditation kama gazeti hali ya kuwa ufuatilii muongozo wa maelekezo yake na taratibu zake basi moja kwa moja itakushinda.

MEDITATION YA KIMWILI

Hii ni safari ya kwanza ya meditation kwa hapa tunatarajia mwenye kuanza kujifunza meditation kuwa na mawasiliano sahihi baina ya yeye na mwili wake kwa ujumla.

Meditation hii itamfanya mwenye kufanya kuwa na Afya nzuri na mwenendo mzuri wa kutambua matukio ya mwili wake na kufahamu thamani yake mwenyewe katika mwili wake.

Mwenye kufanya meditation hii hutegemewa kutengeneza muonekano mzuri wa mwili wake, Afya ya ngozi yake Nuru katika macho yake, makuzi mazuri ya kucha na hata nywele zake kwa uimara na muonekano.

Pia matarajio hapa na matokeo ni kuwa mwenye kufanya meditation ya kimwili basi moja kwa moja atakuwa ni mwenye kuondosha aina zote za maradhi katika mwili wake ikiwa ni pamoja na maradhi yanayotibika pamoja na maradhi yasiyotibika pia.

Mwenye kufanya meditation ya kimwili huonekana kuwa na mwili wenye mvuto kwa jinsia tofauti na yake ikiwa ni pamoja na kuimarisha stamina katika tendo la ndoa. Kuondoa maumivu ya mwili. Uchovu wa mwili na aina zote za sumu mwilini.

Moja kwa moja mwili wa mwenye kufanya meditation hutarajiwa kuwa na kinga madhubuti ambazo hazimtetereshi hata kajika Genetic zake ambazo ndio msingi na msimamo mkubwa wa mwili wa mwanadamu.

Hivyo ikiwa umeamua kufanya meditation ya mwili basi hakikisha kwamba mwili wako huu ni pango ama nyumba yako mpya ambayo ulikuwa unaiishi kila siku bila kujua kama ni yako na hivyo unatakiwa kuiweka sawa na madhubuti kuanzia ndani hadi nje.

Kila aina ya tatizo ambalo lipo katika mwili wako ambalo linakaa katika mwili wako litakuwa eliminated na Meditation ya mwili ili kuuandaa sawa mwili wako katika kupokea hatua ya pili ambayo ni meditation ya akili kisha kumalizia hatua ya tatu ambayo ni meditation ya kiroho.

Kumbuka:
Hivyo ni kawaida kwa mwenye kufanya meditation ya mwili kupata njaa muda mwingi, Kukosa choo na kupata hamu ya vyakula specific ambavyo huenda kwa hali ya kawaida mtu mwingine kutotanani kuvila. Kama vile;
  1. Juice ya ndizi yenye chumvi
  2. Mapera yaliyokaangwa
  3. Nazi zilizo anikwa juani
  4. Samaki wa kukaanga aliyewekewa asali juu
  5. Mchicha wenye sukari n.k

Hivyo mwenye kufanya Meditation ya kimwili mwili wake huanza kudai vitu ambavyo vinaweza kurekebisha tatizo au kujenga mwili sehemu ambayo kuna hitiliafu.

Mfano inaweza kukuijia hali ya kutamani mayai mabichi na ukahisi ni kama una kiu ya mayai mabichi kumbe ikawa ni dawa ya kuweza kutibu eneo la Throat chakra kwa kuwa tu sauti yako kila ukiongea huwa inakwangua ndani bila wewe kujua na baadae huenda ikaleta Ulcers za koo au maeneo ya Esophagus hivyo ukifanya meditation ya mwili hili linaweza kuwa solved in a mysterio ways.

Kuna faida nyingi sana katika mwili wako ikiwa utafanya Meditation ya mwili ambazo siwezi kuandika hapa nikamaliza.

Hivyo moja kwa moja tunaweza kwenda kwenye hatua kwa hatu jinsi ya kufanya meditation ya MWILI

JINSI YA KUFANYA MEDITATION YA MWILI

Tunapozungumzia Utaratibu wa kufanya ya mwili basi moja kwa moja huwa tunalenga uelewa wa mtu na mwili wake kwanza;

Je, kuna faida gani mtu kuuelewa mwili wake mwenyewe?

Zifuatazo ni faida ambazo mtu anaweza kupata kwa kuuelewa mwili wake mwenyewe katika misingi ya Meditation:

  1. Kuongeza utulivu wa usingizi
  2. Kutibu presha
  3. maumivu
  4. Msongo wa mawazo
  5. Kutibu wasiwasi
  6. Kuongeza kinga ya mwili
  7. Kuponya addiction ya aina yoyote
  8. kuponya allergy
  9. kuponya maradhi ya akili
  10. Kuongeza focus
  11. Kuongeza kuona
  12. Kuruhusu kila kiungo kufanya kazi vema.

Nazo hizi ni baadhi ya faida anazopata mwenye kufanya meditation ya Mwili pekee na kama akiwa hana haja ya kuendelea na hatua nyingine nae anakuwa kaamua kufanya tu kwa ajili ya mwili wake au Muonekano wake.

ZIFUATAZO NI TARATIBU ZA KUFANYA MEDITATION YA MWILI

Yoyote mwenye kutaka kufanya meditation ya mwili basi moja kwa moja anatakiwa atambue kwamba kuna meditation aina mbili za mwili.

Moja wapo ni meditation ya Utulivu wa viungo vya mwili na nyingine ni Meditation ya Yoga.

MEDITATION YA VIUNGO VYA MWILI

Ikiwa taratibu yako ni kutaka kufanya meditation ya Viungo vya mwili basi tazama na uele mchoro ufuatao

meditation ya mwili kwa wanaoanza mchoro wa mwili na point zake
Mchoro namba 01.

Awali ya yote fahamu ya kuwa unaoona ni mchoro wa mwanadamu ambao unaonyesha point za mwili wake au kiwili wili chake. Sasa kabla ya kuendelea na mchoro huu tazama mchoro wa pili.

mkao sahihi wa meditation ya mwili kwa wanaoanza kukaa kwa utulivu
Mchoro namba 02.

Katika picha na mchoro namba mbili utaona mkao husika wa meditation ya mwili, Yes huu ndio mkao sahihi wa meditation zote na ndio mwanzo wa meditation.

Mkao huu kwa wengi ni changamoto lakini katika kufanya meditation ya mwili mwanzo wake ni mgumu na baadae ukiweza kuwa awareness na huu mkao basi moja kwa moja utaona mambo yanaanza kwenda jinsi ulivyotarajia.

Hivyo fuata taratibu zifuatazo katika kufanya meditation yako ya mwili siku ya kwanza.

Fahamu ya kuwa hata kama ulikuwa una muendelezo wa meditation zingine ni bora ukaacha kwanza na kurudi hatua ya kwanza kwa maana kuna faida nyingi sana ya kuanza msingi.

MISINGI YA MEDITATION KABLA YA UFANYAJI

Awali katika meditation tulizungumzia meditation ya mwili lakini kutokana na changamoto za wengi inaonekana ni wenye kutala kuanza meditation ya mshumaa ajili ya kupata utulivu jambo ambalo katika taratibu za meditation kuanzia katika meditation ya mshumaa ni muonekano wa kuruka hatua za meditation.

Hii haina tofauti na mwanafunzi wa darasa la kwanza kuanza kujifunza mambo ya darasa la saba.

Ni kweli ataonekana ni mwenye kujua mambo makubwa lakini msingi wake ni mbovu na hii kupelekea baadae katika hatua za juu kuanguka kwa sababu tu kakosa misingi ya kuanza na meditation.

Hivyo mkubali mkatae msingi ni muhimu zaidi kwa yoyote mwenye kutaka kujifunza meditation. Ikiwa mtu anataka kuruka katika meditation na kufanya leo kisha kesho kufaulu basi huyo katika kichwa chake atakuwa anatengeneza Illusion kitu ambacho katika meditation hakitakiwi.

Twende kwa kufuata misingi na taratibu za meditation ili mtu afikie katika mafanikio. Mwa mgumu basi mwisho wake ni rahisi sana lakini mwanzo rahisi mwisho wake ni mgumu sana

Hivyo ajitahidi mwenye kujitahidi na asubiri mwenye kusubiri pitia changamoto nyingi lakini goal yako katika meditation ujue ni nini basi utakuwa umefaulu. Lakini kama unafuata meditation kuona yaliyomo kwenye meditation ni nini maana yake utafeli.

Tuanze na msingi wa meditation kwa pale tulipoanzia hadi sasa. Kwa elimu mliyoisoma ni hii ya awali yoyote yule asiyeweza kuelewa kipengele cha kwanza na sheria ya kwanza katika meditation basi amefail.

Nyote mfahamu ya kwamba kila mmoja wenu humu ana wazo kuhusu meditation lakini hajui ni upi mwanzo na usawa wake.

Wengi wenu wamejaribu kuhusu meditation lakini hawajawahi kufanikiwa hata siku moja kuona meditation ni kitu gani.

FUNGUO YA MEDITATION

Key ya kwanza ya meditation ni Awareness ( Ufahamu/ Uelewa) Na hii key ili yoyote kati yenu aweze kuielewa vema basi kuna sheria zake mbili. Sheria ya kwanza ni: Usilazimishe na sheria ya pili Usisisitize. Do not force and do not concerntrate....

Asilimia 90 ya watu wanaofail katika meditation ni watu ambao husisitiza na kulazimisha ufanyaji wa meditation.

FUNGUO YA MEDITATION

Kila jambo unalotaka kulianza ni lazima kujua funguo au mwanzo wake, Sasa kama funguo ya meditation unataka kufahamu basi jua moja kwa moja funguo ya meditation ni mambo mawili

  • USILAZIMISHE
  • USIWEKE UMAKINI

Funguo hizi hutumika katika kuanza meditation kwa mtu anaetaka kufikia level za juu za meditation hii ninayozungumzia hapa ni meditation kwa ujumla sizungumzii Meditation ya kipengele tulichopo yaani meditation ya Mwili.

Katika hatua za meditation zote 3

  1. Kimwili
  2. kiakili
  3. Kiroho

Zote hizi funguo yake ya mwanzo ni Maneno mawili tu, Kutokulazimisha wala kuwekea umakini. Haya mambo mawili lazima yapaswa kukukaa kichwani kwako na akilini kwako siku zote na iwe ni kama sehemu ya maisha yako nitaelezea mbele ni kwa nini

USILAZIMISHE

Kulazimisha ni ile hali ya kutaka meditation iwe vile unavyotaka wewe, Kama hii ni nafsi ambayo uliyonayo basi jua moja kwa moja unajiosha ubongo wako na kuchafua uelewa wako wote kuhusiana na meditation.

Kulazimisha awali ya yote huanza na akili ya mtu kile kitendo cha yeye kukaa na kuanza kufanya meditation hapo hapo huanza kuwaza wacha nione leo nitapata matokeo gani.

Fahamu kabisa humchukua siku saba mtu mwenye hekima kuweza kuanza kupata matokeo ya zoezi la kwanza la meditation.

Fahamu kabisa humchukua siku 14 mwenye akili timamu kuweza kuanza kupata matokeo ya zoezi la kwanza la meditation.

Fahamu kabisa humchukua siku 21 mtu asiye na mambo hayo mawili juu kupata matokea ya awali ya zoezi la kwanza la meditation.

Ni matokeo gani tunayozungumzia hapo?

Katika matokeo ya kwanza anayopata mtu mwenye kuanza meditation basi ni haya yafuatayo;

  1. Utulivu
  2. Amani
  3. Furaha

1: UTULIVU

Katika zoezi la kwanza la meditation basi mmoja kati ya makundi haya matatu ya watu hupata matokeo haya ya utulivu katika meditation hivyo ndani ya muda tajwa ataanza kujua utulivu kwa maana nyingine tofauti na alivyokuwa akijua awali kuhusu neno utulivu.

Utulivu ni kitu ambacho hujulikana kwa kila mtu kuwa ni hali ya mtu kutulia na hata wengine huchukulia kama mzaha wa hekima kusema neno utulivu kama (Nipo zangu nimechill tu hapa) Akiwa na maana kakaa sehemu katulia.

Fahamu kabisa huu sio utulivu tunaouzungumzia hapa, Utulivu tunaozungumzia hapa nikiandika kwa maneno basi tutarudi pale pale kwenye kuwafundisha kuhusu kusisitiza na hii itapelekea mtu kujitune yeye mwenyewe kutulia hali ya kuwa meditation haitaki hivyo.

Utaexperience utulivu wa mwili wako na utahisi kila kiungo chako ukiwa umetulia basi kimetulia kweli ikiwa ni pamoja na akili na mawazo yako kuweza kutuliza na kuexperience kuhusu utulivu ambao ulikuwa unajua tu neno utulivu na hujui maana halisi ya utulivu.

hivyo katika hatua hii sasa tutakuruhusu kuanza kuendelea na meditation ya kiakili muda wote huu unatakiwa kuzingatia maana ya utulivu kwa vitendo na sio maneno pekee, Hata watu na mazingira yanayokuzunguka yatatamani jinsi ambavyo ulivyokuwa na uwezo mkubwa wa kutulizana.

2: AMANI

Amani ni Jambo kuu la pili katika hatua za kwanza za meditation anapoanza mtu kufanya vipindi vya awali, Ikiwa matokeo ya mwili kuanza kujengeka yanapatikana ndani ya siku kadhaa basi hata meditation matokeo yake hayaanzi hapo hapo isipokuwa mtu atapata maumivu ya kwanza ambayo yamechanganyika na kukosa amani.

Hivyo mtu ambaye hafanyi meditation haijarishi yupo salama au na amani kiasi gani, ukweli ni kwamba kama huna ujuzi wa mwili wako basi huna amani wewe na vitu vingi vitatokea kwa kukushtukiza tu.

Kuamka unaumwa pasipo kujua mwili ulikuwa unakupa taarifa kuwa kwenye mwili limeingia tatizo basi jua taarifa za ugonjwa huanza kuletwa tangu siku au wakati umeingia. Kinachotakiwa mtu ni kuweza kuzungumza vema na mwili wake.

Fahamu ya kuwa matokeo ya pili tangu kuacha kulazimisha meditation basi ni Amani. Amani ni kitu kikubwa kila mtu huota kukipata lakini sio rahisi kama wengi wanavyodhani amani ya mwili haiji kisa tu mtu kaamua ije.

Na kama ingekuwa ni hivyo basi mwanadamu angeweza kuuambia mwili wake utoe ugonjwa ulioingia kwenye mwili wake kwa amani bila vita na ukatoka.

Mwili wako ni taifa kubwa ambalo linahitaji kuongozwa na wewe na ukiuacha ujiongoze wenyewe basi utaleta machafuko makubwa katika taifa hilo.

Uongozi utaharibika, askari watadumaa kufanya kazi kwa bidii, raia kila mmoja atajiambulia anachotaka.

Fahamu ya kwamba ulimwengu wote upo katika mwili wako lakini hauna uwezo wa kuuona kwa sababu tu hujataka kuuona.

Katika hatua ya kwanza niliyowafundisha kuhusu meditation ya mwili na kuelekeza kuwa jambo la kwanza na muhimu ni kuwa kila mwenye kufanya ni lazima kwanza atune mwili wake katika hali ya meditation na kukubali meditation husika anayoifanya kwa ajili ya muendelezo wa mafanikio yake katika meditation.

Mkao husika wa meditation ulikuwa ni kama unavyoonekana kwenye picha.

Mkao husika wa meditation

Mkao huu mmoja wa meditation una mitindo tofauti tofauti ya ukaaji zaidi ya mitindo 20 kwa kutengemea na mkao wa vidole na mkao wa miguu.

Lakini awali ya yote fahamu ya kwamba unapoanza meditation basi ni mkao mmoja tu kama ulivyoonyeshwa pichani ambao ndio mkao wa kwanza wa kukutaka wewe uwe aware na base au chakra ya kwanza ya Mwili wako ambayo hudeal na Surviving.

Nayo ikiwa ni mtu ambaye unaanza kwa mara ya kwanza basi ni muhimu zaidi kuzingatia kuwa ukianza unatakiwa kuanza kwa kufuata taratibu ya misingi ya mavazi na misingi ya hali yako na misingi ya muda wako.

Hitimisho
Meditation inaanza kwa msingi. Ukianza na meditation ya mwili kwa umakini wa utaratibu wake, unajiandaa kwa hatua zinazofuata za akili na kiroho kwa usahihi zaidi.

Shirikisha Post Hii

Facebook Twitter WhatsApp Pinterest

Rakims Spiritual

Rakims Spiritual

Mafundisho ya kiroho, meditation, nguvu ya ndani na maarifa ya siri za maisha.

Soma pia:

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !