Nyota ya Mshale (Sagittarius): Tabia, Mapenzi, Kazi na Mafanikio

Rakims
0

Nyota ya Mshale (Sagittarius)

Tabia, uhuru, mafanikio na maisha ya wenye nyota ya Mshale

Nyota ya Mshale Sagittarius

Utambulisho

Hii ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12. Inahusisha watu waliozaliwa kati ya tarehe 23 Novemba hadi 20 Desemba.

Asili yake ni Moto na inatawaliwa na Jupiter (Mushtara), sayari ya bahati na upanuzi wa maisha.

  • Siku ya bahati: Alhamisi
  • Namba za bahati: 5 na 7

Sifa na Tabia

  • Wapenda uhuru na kujitegemea
  • Wana matumaini makubwa ya mafanikio
  • Wakweli na wazi katika mazungumzo
  • Wapenda kusafiri na kujifunza
  • Wenye moyo wa ukarimu

Udhaifu Wao

  • Kutokuwa na subira
  • Kuzidisha mambo au kutia chumvi
  • Kutopenda kufungwa na sheria
  • Kutojali hisia za wengine wakati mwingine

Rangi na Bahati

  • Rangi kuu: Bluu, Zambarau
  • Rangi za mapenzi: Njano na machungwa
  • Rangi ya mafanikio: Nyeusi na Bluu iliyokolea

Mapenzi

Mshale ni watu wanaopenda uhuru hata katika mahusiano. Wanapenda mapenzi lakini hawapendi kubanwa au kudhibitiwa.

Ni wachangamfu na wenye kupenda, lakini tabia yao ya kupenda uhuru inaweza kuwafanya waonekane kama hawajali sana.

Wanahitaji mpenzi anayeelewa nafasi ya uhuru katika maisha yao.

Kazi na Biashara

  • Sheria na mahakama
  • Ualimu na uandishi
  • Dini na mafundisho
  • Usafiri na utalii
  • Biashara na uuzaji

Afya

Nyota hii inahusiana na nyonga, mapaja na mfumo wa mwili wa chini.

Wanaweza kupata matatizo kutokana na kufanya kazi kupita kiasi bila kupumzika.

Kipaji Chao

Wenye nyota ya Mshale wana kipaji cha kuona mbali na wakati mwingine kutabiri mambo yajayo.

Ni watu wa maono makubwa na wana uwezo wa kufikia malengo yao wanapolenga kwa dhati.

Ushirikiano na Nyota Nyingine

  • Wanaoendana nao: Simba, Punda
  • Wasiopatana nao: Mapacha, Mashuke, Samaki
  • Nyota ya mapenzi bora: Mapacha

Hitimisho

Nyota ya Mshale ni nyota ya uhuru, matumaini na mafanikio.

Unataka kujua nyota yako kwa undani zaidi?

Chat WhatsApp: +255 788 485 293

Email:

Rakimsspiritual@gmail.com

Rakims Spiritual

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !