Nyota ya Samaki (Pisces): Tabia, Mapenzi, Kazi na Maisha

Rakims
0

Nyota ya Samaki (Pisces)

Hisia, ubunifu na maisha ya kiroho

Nyota ya Samaki Pisces

Utambulisho

Hii ni nyota ya 12 katika mlolongo wa nyota 12. Inahusisha watu waliozaliwa kati ya tarehe 19 Februari hadi 20 Machi.

Asili yao ni Maji na sayari yao ni Neptune.

  • Siku ya bahati: Alhamisi
  • Namba ya bahati: 8

Sifa na Tabia

  • Wenye huruma na moyo wa kusaidia
  • Wenye hisia kali na upendo mkubwa
  • Wabunifu na wenye ndoto nyingi
  • Wapole na wenye utu
  • Wenye uwezo wa kuelewa wengine kwa undani

Udhaifu Wao

  • Kukwepa matatizo
  • Kuathirika kirahisi kihisia
  • Kuwa na mawazo yasiyo halisia
  • Kuchanganyikiwa kirahisi

Rangi na Bahati

  • Rangi kuu: Bluu, Kijani, Aqua
  • Rangi za mapenzi: Njano, Machungwa, rangi za udongo
  • Rangi ya mafanikio: Nyekundu

Mapenzi

Watu wa nyota ya Samaki ni wenye mapenzi ya dhati, huruma na kujitoa kwa wapenzi wao bila masharti.

Wanapenda sana mahusiano ya kina na mara nyingi hujitoa kikamilifu katika mapenzi.

Changamoto yao ni kuwaamini sana wapenzi wao na kuwa na matarajio makubwa yasipotimia huumia sana.

Kazi na Biashara

  • Kazi za kusaidia watu (huduma za jamii)
  • Sanaa: muziki, picha, maigizo
  • Ushauri nasaha (Counselling)
  • Kazi za dini na kiroho
  • Kazi za hospitali au huduma kwa wagonjwa

Afya

Nyota hii inahusiana na nyayo na vidole vya miguu.

Changamoto za kiafya hutokea wanaposhindwa kufikia ndoto zao au wanapopata msongo wa mawazo.

Wengine hukimbilia tabia hatarishi kama ulevi au matumizi ya dawa kupita kiasi.

Kipaji

Samaki wana kipaji kikubwa cha ubunifu na uwezo wa kufikiria na kuunda vitu vipya (visionary).

Ushirikiano na Nyota Nyingine

  • Wanaoendana nao: Kaa, Nge
  • Wasiopatana nao: Mapacha, Mashuke, Mshale
  • Nyota ya kusaidia ubunifu: Kaa
  • Nyota bora ya mapenzi: Mashuke

Hitimisho

Nyota ya Samaki ni ya hisia, ubunifu na maisha ya kiroho. Wakiwa na mwelekeo sahihi, wanaweza kuwa chanzo cha faraja na msaada mkubwa kwa wengine.

Unataka kujua nyota yako kwa undani zaidi?

Chat WhatsApp: +255 788 485 293

Email:

Rakimsspiritual@gmail.com

Rakims Spiritual

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !