Nyota ya Mapacha (Gemini): Tabia, Sifa, Mapenzi na Mafanikio

Rakims
0

Nyota ya Mapacha (Gemini)

Sifa, tabia, mapenzi na maisha ya wenye nyota ya Mapacha

Nyota ya Mapacha Gemini

Utambulisho

Hii ni nyota ya tatu katika mlolongo wa nyota 12. Inahusisha watu waliozaliwa kati ya tarehe 21 Mei hadi 20 Juni.

Nyota hii ina asili ya upepo, hivyo huwakilisha mawasiliano, akili na mabadiliko ya haraka.

Sayari Inayotawala

Nyota hii inatawaliwa na Mercury, sayari ya mawasiliano, safari na akili ya haraka.

Sifa na Tabia

  • Wenye akili ya haraka na wabunifu
  • Wana uwezo mkubwa wa kuwasiliana
  • Wachangamfu na wanapenda kujifunza
  • Wanapenda mabadiliko na vitu vipya
  • Wana tabia ya kubadilika haraka

Udhalifu Wao

  • Kukosa uthabiti katika maamuzi
  • Kuwa na tabia ya juu juu
  • Kuzungumza kupita kiasi
  • Kushindwa kudumu kwenye jambo moja

Alama na Asili

Alama ya nyota hii ni Mapacha, inayowakilisha pande mbili za maisha, akili na mawasiliano.

Neno lao tawala ni "Ninafikiria", likionyesha nguvu yao katika fikra na maamuzi ya haraka.

Mapenzi

Wenye nyota ya Mapacha ni watu wa mazungumzo na huvutiwa na uhusiano wenye mawasiliano mazuri.

Wanapenda uhuru katika mahusiano na wanaweza kuchoshwa haraka wakikosa msisimko.

Uaminifu kwao unaweza kuwa changamoto kama hawajapata mtu anayewavutia kiakili.

Kazi na Biashara

  • Utangazaji (Radio na TV)
  • Uandishi na uchapishaji
  • Ualimu na ushauri
  • Biashara za safari na mawasiliano
  • Ukalimani

Sehemu ya Mwili

Nyota hii inatawala mikono, mabega, viganja na mapafu.

Bahati na Rangi

  • Siku ya bahati: Jumatano
  • Namba za bahati: 5 na 9
  • Rangi: Njano, Bluu, Sky Blue

Kipaji Chao

Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa cha mawasiliano, kueleza mawazo na hata kuelewa hisia za wengine kwa haraka.

Hitimisho

Nyota ya Mapacha ni nyota ya akili, mawasiliano na mabadiliko. Watu wake wanafanikiwa zaidi wanapodhibiti mabadiliko yao na kujikita kwenye jambo moja kwa muda.

Unataka kujua nyota yako kwa undani zaidi?

Chat WhatsApp: +255 788 485 293

Chapisha Maoni

0Maoni

Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !